Breaking News

WANGU WA MOYO

WANGU WA MOYO (1,2,3)
imetungwa na Mwalimu Joshua
Ni matumaini yangu u mzima mfuatiliaji wa Joshua blog app karibu katika simulizi ijulikanayo kama wangu wa moyo ,  Naomba pia kwa yoyote ambaye  atakuwa tayari kushirikiana na mimi katika kushare link ya app yetu ya simulizi anitafute kwa namba 0713111547 naomba sana ewe mfuatiliaji wa app yangu yangu usiache kunitafuta ,natamani tuweze kuwafikia wengi zaidi kila siku  ,,,asante sana kwa utakayejitokeza

TUENDELEE ,,,,,,,,,,,,
Ilikua ni jumamosi  caren  aliwahi mapema kabisa chuoni na kupitiliza moja kwa moja leacture room(darasa la chuo) caren alipendelea sana kukaa kiti cha mbele ila siku hiyo haikuwa kama alivyotarajia alivyoingia aliwakuta wanachuo wenzake wameshajaza nafasi za mbele hivyo hakuwa na budi kusogea nyuma kabisa  ya darasa lile ,aneti alichomoa dafatari lake kwenye begi n a kuliweka mezani ,  KIpindi kilivyokuwa kikiendelea  ,kijana mmoja aliingia akiwa amevalia shati jeusi tai nyekundu na koti jeupe  ,kijana huyo alipofika mbele ya darasa wanafunzi wote walimkodolea macho hii  ni kawaida pale mwanafunzi mpya anapojiunga na chuo au anapohamishwa na kuletwa chuoni hapo ,,,wasichana waliokuwa viti vya mbele walianza kumkodolea macho kijana Yule kila mmoja alimshika mwenzake kumwonyesha  ishara kuwa anapaswa atizame ,kijana Yule alimsalimu mwalimu ,,,na mwalimu alimwonyesha kwa ishara kuwa anapaswa ksogea nyuma kabisa ya darasa lile ,,,kijana Yule alipokuwa akielekea nyuma wasichana wote waliokuwa pale mbele waliyageuza macho yao nyuma  na kumsindikiza kaka wa watu alivyokuwa akielekea  kukaa ,kijana Yule alisogea karibu kabisa na caren kisha aka kaa pembeni yake , ```Haya sasa turudishe mawazo yetu darasani sawa ‘’ Ilikikua ni sauti ya leacturer bahati wanachuo wote walianza kumsikiliza mwalimu ,kipindi kiliendelea ,caren alimwangalia kijana Yule aliyekuwa pembeni kwa bahati nzuri alimwona kijana Yule akibabaika sana ,alipomwangalia aligundua kuwa hakuwa na kalama ,caren alichomoa kalamu kwa begi kisha alimkabidhi kijana Yule ,,kijana Yule alipokea kwa furaha sana huku akiachia tabasamu kwani caren alikua ameutambua tatizo lake ,kipindi kilipomalizika kaka Yule alimrudishia caren kalamu yake nakumwambia asante kisha aliondoka zake ,caren alimtazama sana kijana Yule alivyokuwa mtaratibu alimwangalia alivyokuwa anaondoka taratibu ,,,kaka Yule alipofika nje hakuamini alichokutana nacho umati wa wanachuo wasichana walikua wakimsubiri ,,,kijana yule  alishangaa sana kwanini wanamtizama namna ile,,akiwa anashangaa msichana mmoja alimsogelea na kusimama mbele yake kwa mikogo akirembusha macho `` mamboooo kwa jina naitwa lizyyy de pretty lady,sijui wewe mwenzangu nani? Sawa mimi naitwa enock ``waoooooo enock jina kama la anko wangu sijui kama tunaweza badilishana namba ‘’ `enock alimjibu usijali sib ado nipo nitakupatia enock alijibu hivyo na kuondoka zake wasichana walianza  kumzomea lizyy`` hilooooooo wajikuta mrembo eti kila kijana akija ni wa kwako haya sasa leo umekaziwa mpaka namba tena tumerekodi kumbe muda ule ule  wakiwa wanaongea getrude alikua  akirekodi alikua amejibanza nyuma ya uzio wa chuo kile ,,,, wasaichana wenzake yaan mashoga zake na lizzy walimcheka sana na kumwaribia lizzy siku yake ,basi baada ya kumcheka kila mmoja alitawanyika
Enock ni mzaliwa wa Morogoro ,,,ila kutokana na matatizo kidogo katika familia yao aliweza kuamishwa kutoka chuo cha Dodoma na kuletwa chuo kimoja morogoro kijulikanacho kama patco,,,,enock alishangazwa sana na wanawake wa patco maishani mwake hakuamini kama mwanamke anaweza anza kumtongoza  au kumshobokea mwanaume ila kwa siku hiyo aliona live bila chenga ,,….
Usiku huo  enock alimwaza sana msichana Yule aliyemsaidia kalama wakiwa leacture(darasani) alimwaza ni ukarimu wa jinsi gani alikua nao aliendelea kumwaza mpaka akapotelea usingizini
Kesho yake enock aliamka asubuhi kama ilivyokuwa kawaida aliwahi sana chuoni hakutamani kuchelewa chuoni ,siku hiyo alibahatika kukaa mbele kabisa ya darasa ,akiwa amekaa alitupa jicho pembeni yake alishangaa kumwona caren binti aliyekuwa amekaa nae jana yuko pembeni ,alimtupia jicho la kiwizi kwa bahati nzuri caren naye alimwona walipungiana na kusalimiana kisha kipindi kiliendelea
Kipindi kilipoisha kama kawaida enock aliondoka zake ile ametoka nje akakumbana na lizzy ana kwa ana ``hellow enock wait plizzzz’’ nataka tuzungumze ,,enock alitulia kimya ila akiwa anamsubiri caren alifika mahali pale ,enock nini shida mbona upo mwenyewe  ,enock moyo wake ulipasuka paaaaaa!!!! Aliposemeshwa kwa sauti ya upole na caren sauti ile ilipenyeza ndani ya moyo wake na kusababisha tetemeko la ajabu alimjibu kwa heshima zote ``Yule dada kaniambia nimsubiri hapa ‘’ caren alipogeuza kichwa nyuma alimwona lizzy akija kwa spidi ya ajabu caren alijib `` sawa enock keshoo ‘’ alijibu akiwa anondoka ,ila akiwa anaondoka enock aliuvuta mkono wake ,lizzy nae alipofika pale alishindwa kustahimili kumwona enock akiwa ameshikilia mkono wa caren alimsukumiza chini careni kwa nguvu ,,,,…..caren alidondoka pembezoni mwa uzio  ule ,………
  JE ENOCK ATAFANYAJE ?????
CAREN NAE  JE??????

MAONI 0713111547
KAMA WEWE NI MPENZI WA SIMULIZI ZANGU NAOMBA USISITE KUWASILIANA NA MIMI TUSHIRIKIANE KATIKA KUSAMBAZA LINK YA APP YETU  MUNGU AKUBARIKI

WANGU WA MOYO (02)
Kipindi kilipoisha kama kawaida enock aliondoka zake ile ametoka nje akakumbana na lizzy ana kwa ana ``hellow enock wait plizzzz’’ nataka tuzungumze ,,enock alitulia kimya ila akiwa anamsubiri caren alifika mahali pale ,enock nini shida mbona upo mwenyewe  ,enock moyo wake ulipasuka paaaaaa!!!! Aliposemeshwa kwa sauti ya upole na caren sauti ile ilipenyeza ndani ya moyo wake na kusababisha tetemeko la ajabu alimjibu kwa heshima zote ``Yule dada kaniambia nimsubiri hapa ‘’ caren alipogeuza kichwa nyuma alimwona lizzy akija kwa spidi ya ajabu caren alijib `` sawa enock keshoo ‘’ alijibu akiwa anondoka ,ila akiwa anaondoka enock aliuvuta mkono wake ,lizzy nae alipofika pale alishindwa kustahimili kumwona enock akiwa ameshikilia mkono wa caren alimsukumiza chini careni kwa nguvu ,,,,…..caren alidondoka pembezoni mwa uzio  ule ,………
Caren alisimama taratibu na kujifuta vumbi hakuwa na muda wa kupoteza wala muda wa kubishana na mtu taratibu aliondoka kuelekea nyumbani ,enock alirudisha macho mna kumwangalia lizzy hakuwa na la kumfanyia haraka alimkimbilia caren  huku akihema `` caren samahani jamani kwa yaliyotokea huyu hata simjui nisamehe sana sijui msichana huyu ana lengo gani kukupigia caren kwa sauti ya upole alijibu `` usijali  hamna tatizo  usijali ‘’ ghafla gari lilifunga breki mbele ya enock na caren `` waooooo caren ingia ndani tuondoke ‘’ alikua ni kaka wa  caren akirudi kutoka kazini .caren alimwaga enock na kupanda ndani ya gari  kisha waliondoka enock alibaki akilitizama gari lile lilivyokuwa likichanja mbuga ,alipoyarudisha macho yake aligongana ana kwa ana na lizzy aliyekuwa mbele kidogo ,,enock alipoona lizzy anamtazama aligeuka upande mwingine kisha kuanza kuondoka ,,lizzy  aliita kwa nguvu `` enockkkkkkkkkkk please wait’’ enock kwa jinsi lizzy alivyomkasirisha aliondoka moja kwa moja  ,,lizzy alijipiga piga mikono yake kwa hasira nakuondoka zake
Caren alipofika nyumbani alipitiliza chumbani  moja kwa moja na kujitupa kitandani ,uchungu ulimshika alilia sana alikumbuka jinsi  lizy alivyompiga kofi aliwaza kosa liko wapi ila hakupata jibu ,,alilia sana ila baada ya muda uchungu ulimwisha akaanza kufikiri kwanini hali ile ilikua vile wazo lilimjia kuwa wenda kuongea kwake na enock ndio tatizo ,aliwaza hivyo ila hakuwa na hakika na jibu lake alipitiliza nje nakuendelea na shughuli zake nyingine hakutamani kufikiria zaidi juu ya suala hilo
Ni Wiki moja toka tukio la caren kupigwa na lizy ,enock kutokana na uwezo wake mkubwa darasani mwalimu wao alimpongeza sana na kumteua kuwa kiongozi wa wanachuo wenzake yoyote Yule mwenye tatizo alipaswa kumuona enock darasa zima walipiga makofi kwa uteuzi wa upendeleo uliofanywa na mwalimu,,enock alikabidhiwa madaraka hayo hivyo kazi  ilianza
Upande wa pili lizzy alijaribu kila mbinu kumteka kimapenzi enock ila mbinu zote ziligonga mwamba enock huyo aliyedhania  awe mpenzi wake ndio kabisa mawazo yake yako mbali hana habari na mtoto  wa mtu ,,,,
Ilikua ni siku ya jumatano baada ya vipindi kila mmoja alitawanyika kuelekea nyumbani lizzy alitamani sana siku hiyo apajue nyumbani kw aenock hivyo aliamua kujitoa mwanga amfuatilie nyuma ila kabla hajafanya hivyo aliwafuata mashoga zake na kuwaeleza ya moyoni ,kwa kawaida lizzy alikua anajisikia sana na siku zote aliamini hakuna mwanaume anayeweza kumkatalia ,,marafiki zake walilijua hilo vyema ,,,,lizy aliwafuata mashoga zake aisha ,mwaju pamoja bertha aliwaeleza haya `` shoga zangu unajua nimeshindwa kabisa kumpata enock’’   kabla hajamaliza sentensi  bertha  alicheka kwa nguvu ```hahahah makubwa  wewe si ndo ulitwambia ni kivuruge wa mtaa a.k.a grisi hakuna chuma kisicholegea kwako eti hata mwanaume awe mgumu kama mfupa anakuwa mpole haya mama imekuaje tena’’ lizy alimzaba berta kibao cha mgongo paaaaaah!!!! ``nakwambia  fuata yako mwanamke wewe nilidhani wewe rafiki kumbe wewe wale wale wanafiki’’  aisha alidakia `` shoga msamehe, sasa shoga angu tufanyeje wewe cha msingi mtokee kwao unajua sometimes wanaume wanavimitego vyao wenda anakupima ajue je?unampenda kweli’’  waooooo shoga ata mimi nawaza hivyo sasa ngoja nimtokee kwao
Wakiwa wanaongea ghafla enock alipita karibu yao `` hellow mko salama ‘’ alisalimia na kuondoka
Aisha alimwambia lizzy haya mama kazi kwako mfuate nyuma huyo usicheleweshe sasa
Lizzy alianza kumfuata enock nyuma alitembea akinyata ili enock asijegeuka nyuma na kumwona

JE NINI KITAENDELEA
MAONI 0713111547


WANGU WA MOYO (3)
NA JOSHUA SHAO
cha msingi mtokee kwao unajua sometimes wanaume wanavimitego vyao wenda anakupima ajue je?unampenda kweli’’
``  waooooo shoga ata mimi nawaza hivyo sasa ngoja nimtokee kwao ‘’
Wakiwa wanaongea ghafla enock alipita karibu yao `` hellow mko salama ‘’ alisalimia na kuondoka
Aisha alimwambia lizzy haya mama kazi kwako mfuate nyuma huyo usicheleweshe sasa
Lizzy alianza kumfuata enock nyuma alitembea akinyata ili enock asijegeuka nyuma na kumwona
Enock aliyekuwa mbele mita kadhaa alikua anatembea kwa furaha sana huku akiimba wimbo mmoja wa msanii mmoja wa marekani wimbo aliokuwa akiupenda wimbo uitwao ``To be with you ‘’ ulioimbwa na Mr big aliendelea kuimba kwa furaha huku aakichaja mbuga ,,enock alipoongeza mwendo lizzy nae aliongeza spidi yake ,enock alishikwa na machale na wasiwasi kuwa kuna mtu anamfuatilia kwa nyuma aligeuza shingo nyuma wakati anageuza lizy nae alijibanza kwenye uzio wa maua ,enock alipoona kuwa hamna mtu anayemfuatilia alipata matumaini sana hivyo aliendelea na safari yake ,,enock alifika nyumbani kwao na kupitiliza moja kwa moja  ndani ,,nyumbani kwa enock kulikuwa na geti moja leupe hivyo lizzy alifurahi kupajua hapo alitoa simu yake kubwa (Samsung galax) kisha alichukua picha kadhaa nje ya jengo la wakina enock alifanya hivyo kusudi siku nyingine akirudi asijepotea alipomaliza kupiga picha lizzy alivuta pumzi kwa nguvu kisha alijipongeza mwenyewe na kuachia tabasamu la furaha alirudi nyumbani kwao akiwa na furaha ,alijisemea moyoni kwa kuwa nimeshapajua kwao siku ya weekend (mwisho wa wiki)  nitamfanyia ziara ya kushtukiza naamini nitafanikiwa tu
Enock alipofika nyumbani alikua amechoka sana na alikua mwenye mawazo chungu nzima alipitiliza chumbani alichukua taulo yake na kwenda kuoga ,alipomaliza kuoga alielekea dining (sehemu ya kulia) kwa ajili ya chakula ,alipofika dining alimkuta mama mdogo wake yupo ameketi anamsuburi `` woooooo my son ,handsome wangu pole kwa masomo baba ‘’
`` asante mama nashukuru nyumbani mmeshindaje ‘’
`` yaan tuko salama kama unavyotuona ‘’
Mama mdogo wa enock ajulikanae kama Catherine alimnawisha enock mikono kisha alimpakulia chakula na wote kwa pamoja walianza kula huku wakiendelea na  mazungumzo
Nyumbani enock alikua akiishi na mama mdogo wake pamoja na dada yake tu ,wengine wote ikiwemo baba na mama walikua dare s salaam kikazi  hivyo kampani yake akiwa nyumbani ni mama mdogo na dada yake aitwaye  Doreen
Baada ya kula enock alimwaga mama mdogo wake na kumwambia kuwa amechoka anahitaji kupumzika 
`` mama angu nimechoka sana ngoja nikuache mama ‘’
`` mhhh derik mna kila siku wewe mchovu tu duuuh’’
``Siku hizi sikuelewi mwanangu’’
`` mama nimechoka kweli siunajua masomo tena’
Enock alielekea chumbani  kwake na kujipumzisha kitandani akiwa kitandani mawazo yalikua yalikua yameziteka akili muda wote alikua akimfikiria  sana caren ,alimwona caren kama malaika mwanamke mpole sana ,matukio mbali mbali yalizunguka akilini kwake alikumbuka siku ile  alivyofika chuoni kwa mara ya kwana caren alivyomsaidia kalama ,,,pia alikumbuka siku ile lizzy alivyompiga kibao caren ila caren hakujibu lolote aliondoka taratibu na kuishia zake ,,,kumbukumbu hizi zilizunguka sana kichwani  mwa enock alijikuta akitoa machozi mwenyewe kwa jinsi alivyouona upendo wa caren alimwona caren ni msichana mtaratibu asiye na doa lolote ,,,,japo kwao walikua ni matajiri sana ila caren alikua ni mnyenyekevu sana na asiye na makuu ,,enock aliendelea kumfikiria caren mpaka akapotelea usingizaini akiwa katika mawazo yake,,,,
Usiku wa manane enock akiwa katika usingizi mzito ndoto ya kimahaba ilimjia ,aliota yupo sehemu fulan hivi tulivu,  sehemu iliyozungukwa na miti mingi ya kivuli na majani laini kwa chini enock alikua na patano na bibie caren  hivyo alikaa chini huku akimsubiri mpenzi wake wa moyo afike ,enock alikua ameshikilia ua zuri mkononi tayari kumkabidhi bibie mapema tu atakapofika ,,enock alisubiri sana ila ilipopita kitambo alimwona caren akija kwa mbali akiwa amevalia jinsi nyeusi na koti jekundu kwa jinsi caren alivyokuwa akimfuatilia enock ,,enock alimwona caren kama malaika ,tabasamu zuri la caren lilimfanya enock kujiona mwanaume mwenye bahati sana duniani ,,caren alimsogelea enock alinyoosha mikono yake na kumkumbatia enock kwa nguvu,…… Ghafla enock alizinduka katika ndoto alijikuta ameukumbatia mto wake uliokuwa pembeni huku akitetemeka mdomo wake ulikua umegusana na mto ,,kwa hasira enock  alitukana kwa nguvu ```upumbavu gani huuu careen jamaniiiiiiiiiiiii ‘’’ kelele aliyotoa enock ilipitiliza mpaka chumbani kwa mama mdogo wake ,kwa haraka  mama mdogo Catherine alikimbilia chumbani kwa enock ,,,enock alikua kama amechanganyikiwa alirudia tena kwa nguvu  ``carennnnnnnnnn ‘’


Je nini kitaendelea ................................

simulizi hii ipo tayari vipande vyote 32 soma mwanzo mwisho kwa gharama nafuu mno ya shilingi 1000 lipa kwa namba 0742873299 jina la mpesa martha shayo ukimaliza 


GUSA HAPA KUPEWA YOTE 







No comments