Breaking News

SIMULIZI


KUFA NIACHIE WANANGU (1&2)
mwalimu joshua
0713111547 Whatsapp
Irine hakuamini kama mume wake wa ndoa anaweza kumfanyia uhuni na ukatili namna hiyo ,irine aliyakumbuka maneno ya mama yake aliyokuwa akimwambia
``Mwanangu kuwa makini sana na wanaume sio watu wa kuwaamini asilimia mia ,leo atakupenda ila ikifika kesho anaweza kukugeuka kabisa usiamini ni yeye ,haijalishi  umeishi nae miaka mingapi’’
Ilisikika sauti ya Kelvini mume wa irine
``We mwanamke mpumbavu toka hapa kabla sijakupasua pasua muone kwanza na tumbo yake iliyovimbiana kama kiroba cha mchele’’
Irine uvumilivu ulimshinda alimwambia mume wake
``Baba jaena unamkosea Mungu huu ujauzito wako wewe unaufananisha nakiroba  cha mchele ‘’
Kelvini kwa hasira aliropoka hakujali kuwa wanae Jaena na Simoni wanasikia
``Mpuuzi wewe nani kakwambia ubebe mimba ,kazi kubeba mimba kama nguruwe tu sasa sikia we mwanamke kwa taarifa yako mimi sikutambui wewe na hicho kidubwasha ulichobeba ,utajua utakipeleka wapi hakuna  aliyekutuma kubeba mimba sawa ‘’
Irine alitoa kelele iliyoambatana na uchungu mkubwa
                ``Mume wanguuuuu leo unakana mimba yako tena mbele ya watoto wako jaena na simoni ,Mungu anakuona nakwambia ‘’
Kelvini alikuwa akipasua kuni alishika kipande cha ukuni kwa hasira alimfuata mke wake na kuanza kumtoboatoboa tumboni bila huruma huku akitamka maneno ya kashfa sana
Irine alilia kwa uchungu sana
SONGA NAMI………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Miaka takribani kumi na tatu iliyopita Kelvini alivutiwa sana na binti wa mzee Priscuss,alitamani sana amfanye irine kuwa mkewe ,alipambana sana kila mara kumwinda irine mchana na usiku kuhakikisha irine atakuwa mkewe ,Kelvin alipata changamoto kubwa sana kwani ,irine alikuwa amechumbiwa na wanaume wengi sana kiasi cha kumfanya kelvini kuvunjika moyo na kuona itakuwa ni ngumu sana kwake  kuweza kufanikiwa kumpata irine
Kama ni kwa uzuri irine amejaliwa sana urembo siyo sura tu hadi tabia yake ilikuwa ni njema sana na yenye kuvutia mno
Mzee Priscus kwa kuona jinsi binti yake anavyonang’aniwa sana na vijana mtaani pale ,aliona huu ni wasaa mzuri sana wa kujipatia fedha za kutosha
Alichoamua kufanya baba irine alitangaza ``Kwa anaetaka kumwoa binti yangu gharama ni shilingi milioni moja mahari pamoja na ng’ombe mbili pia anijengee nyumba ndogo vyumba viwili
Alipotangaza hivyo vijana kama wote walikimbia alibaki kelvini tu ,kelvini hakuwa na hela ila alichokifanya aliuza sehemu ya shamba lake alilopewa na baba yake kisha alikwenda moja kwa moja kulipa mahari
Alipomaliza kulipa mahari alikabidhiwa rasmi binti Yule ,irine hakuwa na kipingamizi alikubalina na kelvini kwani ndie mwanaume pekee aliyemgharamikia kwa gharama kubwa bila kujali chochote kile
Kelvini alifanya maandalizi ya haraka ndani ya mwezi huo huo alifunga harusi kubwa sana iliyotikisa mtaa mzima ,baada ya harusi hiyo wapendanao hao walianza maisha yao
Siku za mwanzo kelvini alimpenda sana mke wake alimtunza na kumlinda kama malaika ,irine alifurahishwa sana na mume wake alimwahidi kumpenda na kumtumikia daima
Ndan ya mwaka huo huo irine alibeba mimba na kujifungua mtoto wa kike waliyempa jina la Jaena
Baada ya mwaka mmoja na nusu alizaliwa simoni ,haikupita miaka mitatu alizaliwa Erick jumla walikuwa ni watoto watatu waliofuatana
Kelvini alipambana sana kuwatunza watoto wake ,ilifika hatua mke wake aliamini kabisa kelvini ni baba sahihi kwa wanae
Jirani kabisa na ireni aliishi dada mmoja ajulikanae kama Shamim ,miaka yote shamim hajawahi kuolewa maisha yake yote ni kudanga na kutembea na waume za watu
Shamim alikuwa na kigenge kidogo cha mboga mboga na viungo alikua anakitumia kama chambo ya yeye kuonekana anafanya kazi ila haikuwa kweli alikuwa ni Malaya na mdangaji original ,hela za kigenge na maisha ya fahari aliyokuwa nayo ni vitu viwili tofauti
Siku moja kelvini mume wa irine alipokuwa akitoka kazini alipita gengeni kwa shamim kwa ajili ya kunua viungo na mboga za kupeleka nyumbani ,alipofika gengeni pale alimsalimu shamim
``Hellow vipi dada’’
Shamimi huku akizungusha jicho kwa mahaba na mbwembwe nyingi alijibu
``mambo baba jaena nikusaidie nini mwaya’’
``Nisaidie karoti nyanya bamia pamoja na samaki’’
Shamim aliingia ndani alichukua dawa yake na kupaka mikononi haraka haraka ,shamim alipewaga dawa na mganga mmoja aitwae mgulula huyu ni mganga anayetoa dawa za mvuto wa kishetani mwanamke akikupa mkono tu hunasuki utatoa hadi vishilingi ulivyonavyo unaweza kuuza hadi shamba kisa yeye
Kelvini akiwa nje ya genge alisema
``hey shamimi mbona unachelewesha chenji au nije baadae ‘’
Shamim alikuwa akimaliza kujipaka mafuta yale
Alipomfikia kelvini kwanza alirembua kama jini alinyoosha mkono na kumshika
Kelvini aliingiwa na kitu cha ajabu msisimko ulimpanda alimwona shamim kama malaika ,shamim alibaki akimdolea macho kelvini anavyobabaika alijua hapa tayari dawa ishafanya kazi
Huwezi amini kelvini muda huo huo alizama ndani ya kijumba cha kahaba Yule hela zote  alizokuwa amekusanya wiki nzima aligawa karibu nusu yake ,walipagawa na kuingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba
Baada ya hapo kelvini hakutamani hata kurudi nyumbani ila shamim alimwambia
``Kipenzi peleka basi mboga utakuja baadae ‘’
Kelvin alimkiss shamim na kuondoka ila akili yake ilikuwa imenaswa
Maskini Kelvin alivyofika nyumbani kama ilivyokawaida mke wake alimkimbilia akiwa na wanae
``BABA BABA WAOOOOOOO MUME WANGU’’
Kwa haraka mke wake na kelvini aliona mabadiliko mume wake hakuwa na raha nae ,kwa kulazimisha irine alimkumbatia mume wake ila huwezi amini irine alipigwa kofi zito usoni
``PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAH’’
Jaena na simony walikimbia kwani toka wamezaliwa hawajawahi muona mama akipigwa
Je nini kitaendelea
Irine atafanyaje ??? kelvini nae Je????
Simulizi hii ipo tayari soma mkasa huu wa kusisimu kwa sh 1000 utaungwa na  kundi langu la simulizi za kusisimua karibu sana ujifunze mengi pia ukinunua hii utapewa na ofa ya simulizi nyingine nzima mbili ,simulizi za Joshua tunakupenda lipa kwa mpesa 0742873299  ukimaliza tuma meseji tayari kisha njoo whatsapp kwa o713111547

KUFA NIACHIE WANANGU (2)
Kelvini aliingiwa na kitu cha ajabu msisimko ulimpanda alimwona shamim kama malaika ,shamim alibaki akimdolea macho kelvini anavyobabaika alijua hapa tayari dawa ishafanya kazi
Huwezi amini kelvini muda huo huo alizama ndani ya kijumba cha kahaba Yule hela zote  alizokuwa amekusanya wiki nzima aligawa karibu nusu yake ,walipagawa na kuingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba
Baada ya hapo kelvini hakutamani hata kurudi nyumbani ila shamim alimwambia
``Kipenzi peleka basi mboga utakuja baadae ‘’
Kelvin alimkiss shamim na kuondoka ila akili yake ilikuwa imenaswa
Maskini Kelvin alivyofika nyumbani kama ilivyokawaida mke wake alimkimbilia akiwa na wanae
``BABA BABA WAOOOOOOO MUME WANGU’’
Kwa haraka mke wake na kelvini aliona mabadiliko mume wake hakuwa na raha nae ,kwa kulazimisha irine alimkumbatia mume wake ila huwezi amini irine alipigwa kofi zito usoni
``PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAH’’
Jaena na simony walikimbia kwani toka wamezaliwa hawajawahi muona mama akipigwa
Irine alishangazwa sana na mume wake kwani hakujua amempigia kwa sababu gani ,irine alisogea pembeni kwa uoga mkubwa alisema
``Mume wangu nimekukosea nini baba ‘’
Kelvini alimfuata kwa haraka huku akitaka kumpiga tena irine alitambua hili na kuondoka kuelekea jikoni kwa ajili ya kumwandalia bwana ake chakula ,ila moyoni alikuwa na uchungu sana kwani hakujua ni sababu ipi Imempelekea bwana wake kumpiga
Upande wa pili kelvini alikuwa kama mwehu kila akifunga macho alikuwa akimwona shamim mbele yake ,shamim aliijaza akili yake na kuziteka fikra zake ,hakika dawa za kichawi ni mbaya sana na zimekuwa sababu ya kuharibu ndoa za watu
Irine alimpakulia bwana  ake chakula na kukipeleka alipo kwa heshima kabisa alimwambia
``Mume wangu karibu chakula ‘’
Irine alikuwa ameaanda ugali na mchuzi wa samaki
Kelvini kwa hasira alimtazama mkewe na kusunya kiume ,kisha alimkata jicho moja la dharau sana huku akisema
``Nini hiki’’
Irine alihisi kuchanganyikiwa kwani siku hiyo alikua ameendaa mchuzi mzito sana wenye nazi na makorokocho kama yote
Akiwa anajishauri cha kumjibu mume wake alimwagiwa mchuzi ule usoni ,kwa kweli kelvini alifanya kitendo kibaya sana kwa mkewe kibaya zaidi jaena na simony walikuwa pembeni wakiangalia televisheni ,
Baada ya kufanya hivyo kelvini aliingia bafuni alioga bila hata ya kumsemesha mke wake aliondoka moja kwa moja kurejea kwa mwanamke kahaba shamim
Upande wa pili shamim akiwa chumbani alikuwa akicheka sana huku akisema
``HAHAHA mery ,na Jesca kila siku mmekuwa mkimsifia irine mnasema ameolewa na mwanaume anayempenda asiyechepuka haya sasa nipo na kelvini na kwangu anasuki hadi niamue mimi kwasababu mimi ndio injinia mwenyewe shamim alijitapa mno
Irine mke wa Kelvin alilia sana ,alilia kwa uchungu na kwikwi kwani aliyomfanyia mume wake ni mambo ya ajabu sana na hakuamini kabisa kama baba Jaena mume wake aliyekuwa akimpenda kwa dhati anaweza kumfanyia kitu kama hicho
Jaena alipomwona mama yake alimfuata na kuanza kumbembeleza wote kwa pamoja walianza kulia simony nae alisikitika sana kutokana na kuwa yeye ni mtoto wa kiume alijikaza kiume ila hakupendezwa hata kidogo alichokifanya baba yake
Shamim akiwa ndani alisikia mlango ukigongwa ,hakujua ni nani amegonga moja kwa moja aliitika kwa sauti ya madaha ingia
Alishangazwa sana kwani aliyeingia alikuwa ni kelvini
``Haaaa ushafika kwa mkeo kweli wewe si sasa hivi tu umetoka hapa’’
``hamu ya chakula sina shamim nakuwaza wewe’’
Shamim alicheka kwa kebehiii
``hahahaha makubwa unaniwazaje sasa kelvini’’
``We hujui tu nakupenda sana natamani hata nimfukuze Yule mdoli kule nyumbani nibaki na wewe ‘’
``Aseee ukifanya hivyo nitajua unanipenda kweli ‘’
``We ngoja na cha ajabu kwa sasa naona kama anakiujazito mwanamke anazaa kama panya ananiletea mtoto wanne wa kupeleka wapi sasa huyu lazima nimtimue tuende tukatawale kule kwa raha zetu ‘’
Shamim alicheka aliikubali sana dawa ile alijua ile dawa ina nguvu kupita maelezo alikumbuka kitu kimoja alichoambiwa na daktari ambacho akikifanya tu mwanaume anaweza mpa hadi kadi yake ya benki na kumwachia
Shamim alipokumbuka hilo alinyanyuka na kuelekea  jikoni aliandaa chai haraka haraka alipomaliza
Alivua nguo zake kisha akachukua nguo yake ya ndani (chupi) akaiweka juu ya kikombe cha kelvini kisha akaanza kuchuja chai kwa kutumia nguo yake ya ndani ,alitumia nguo yake ya ndani kama chujio
Akiwa anafanya huo ushetani kwa siri ghafla alishtuka kumwona kelvini akiwa mbele yake ,huwezi amini kelvini alikuwa amemfuata shamim jikoni …………………..
Je Kelvin atafanyaje >……………………………………………………………………………..





LIPA SHILINGI ELFU MOJA KUSOMA SIMULIZI NZIMA
LIPA KWA 0742873299

GUSA HAPA KUSOMA WHATSAPP

No comments